🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓
Uongozi wa Shule unawapongeza kwa dhati kwa matokeo haya wanafunzi wetu wa kidato cha Nne 2020.Mungu na awatangulie katika safari yenu ya kitaaluma kwa wale mtakaoyatumia kujiendeleza kielimu zaidi na hata wale mliofanya vibaya msikate tamaa maana bado mnayo fursa kubwa sana katika maisha.
Shukran kwa Walimu,wazazi na wale wote walioshirikia katika kuhakikisha Bunda Secondary inazidi kupanda juu zaidi katika taaluma.Hakika matokeo haya yatakua ni chachu ya kuboresha zaidi na zaidi taaluma ya shule yetu.
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏
PONGEZI nyingi ziwaendee wanafunzi wa kidato cha pili ambao nao pia kwa juhudi kubwa wamefanya vizuri.Tunawakaribisha tena kwa Mikono miwili katika kuendelea na Ngwe nyingine tena kwa masomo ya Kidato cha tatu Tunawaahidi kua nanyi bega kwa bega katika kuwaandaa ili mje kufanya vyema kabisa katika mtihani wenu mwakani.Maana siku zote MAVUNO yaliyobora hutokana na MAANDALIZI yaliyobora Pia.TUNAWAPENDA SANA.
Mwisho kabisa Pongezi za kutosha ziwaendee WALIMU,WAZAZI/WALEZI na washika dau wote walioshikana nasi Bega kwa bega mpaka hapa tulipo.Mchango wenu bado unahitajika sana.
TUNASEMA NIDHAMU NI USHINDI NA MAPAMBANO YANAENDELEA.
UNGANA NASI KATIKA UKURASA WETU WA FACEBOOK
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏