Saturday, June 17, 2017

WASHINDI WA KONGAMANO LA MALIHAI 2017

 Bunda sekondari waibuka kidedea katika kongamano la Mazingira la mwaka 2017,
Kongamano hilo lilifanyika tarehe 2-5 June 2017 kwa hisani ya MALIHAI kanda ya ziwa,kongamano hilo lilifanyika Wilayani Serengeti shule ya sekondari ISENYE.
Kikundi hiki cha wanafunzi wa MALIHAI  kilifanya vizuri katika kongamano hilo hasa katika maonesho na uhifadhi wa mazingira ya shule ya sekondari Bunda na kufanya kuwa washindi wa kwanza.
Wanafunzi hao walijipatia zawadi mbali mbali kama inavyoonekana pichani.Zawadi ambazo ziliwasilishwa shuleni ili kuendeleza harakati za utunzaji na uhifadhi wa mazingira ya shule.
Hata hivyo wanafunzi hao waliwashukuru sana walimu wao Madam Levenda E.K na Mwl Afti Mikingi kwa kuwapa mwongozo mzuri.

Wanafunzi wa Malihai Bunda Sekondari wakitoa maelekezo juu ya matumizi ya "Greenhouse" katika maonesho ya kongamano hilo.

No comments:

Post a Comment