BLOGU HII NI MAALUM KWA MASUALA YA TAALUMA YAHUSUYO BUNDA SEKONDARI.MAONI YENYE LUGHA ZISIZO NZURI YATAONDOLEWA.KARIBUNI KWA MAONI NA USHAURI. "NIDHAMU NI USHINDI"
Friday, June 7, 2019
Thursday, June 6, 2019
WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO TOKA NA KUJIUNGA BUNDA SECONDARY SCHOOL 2019/2020
WALIOCHAGULIWA TOKA BUNDA SECONDARY SCHOOL 2019/2020Tunapenda kuwapongeza vijana wetu wote waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano kwa tahasusi mbali mbali,pia wale waliochaguliwa kujiunga na vyu mbali mbali na bila kuwasahau wale ambao hawajachaguliwa na wakaamua kujiunga na masomo ama vyuo mbalimbali binafsi,tunaamini watafanya vizuri huko waendako.Na kwa wale mlioamua kuikamilisha safari ya Elimu na kuamua kujiunga na shughuli mbali mbali za ujasiliamali nanyi pia tunawatakia kila lakheri.
Kwa wale mliochaguliwa kujiunga na Bunda secondary kwa tahasusi zetu za HGK,HGK na EGM karibuni sana,Bunda secondary ni kisima cha maarifa hakika hamtatoka kama mlivyokuja tunawakaribisha sana.Kwa taarifa zaidi wasiliana na uongozi wa shule ama kwa Barua pepe bundahighschool@gmail.com
Mzazi mlezi mlete mwanao aliyechaguliwa Bunda secondary maana kwetu " NIDHAMU NI USHINDI"
WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA BUNDA SECONDARY KIDATO CHA TANO 2019/2020
Nanyi mliopita Bunda secondary tunaamini huko mliko mnaendelea kua mabalozi wazuri wa shule yetu pendwa kwa kuitangaza kwa mazuri yote.

ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA ELIMU YA KATI NA VYUO VYA UFUNDI JUNE 2019

Saturday, June 1, 2019
HALMASHAURI YA MJI BUNDA KINARA TENA UMISSETA 2019 MARA
Mashindano ya UMISSETA mkoa yalianza tarehe 29/05/2019 na kuhitimishwa tarehe 01/06/2019 katika viwanja vya shule ya sekondari Bunda. Mashindano haya yalihusisha halmashauri tisa za mkoa wa Mara ambazo ni Musoma manispaa,Musoma vijijini,Rorya,Bunda wilaya,Bunda Mji,Butiama,Tarime Mjini,Tarime vijijini na Serengeti.
Halmashauri zote hizi zilileta timu za michezo mbalimbali zikiwemo fani za ndani.
Washindi mbalimbali toka halmashauri mbalimbali waliibuka na kujinyakulia zawadi kemkem zilizokuwa zimeandaliwa ikiwemo Vyeti na vikombe.
Halmashauri ya Bunda iliibuka kuwa bingwa wa Jumla katika mashindo ya mwaka huu ikiwa ni mara mbili mfululizo na kutwaa vikombe mbalimbali kama ifuatavyo kikombe cha mpira wa mikono wasichana na wavulana mshindi wa kwanza, kikombe cha mpira wa miguu wasichana mshindi wa kwanza, kikombe cha mpira wa kikapu wasichana mshindi wa kwanza, kikombe cha riadha wasichana mshindi wa kwanza, kikombe cha kikapu wavulana mshindi wa pili na kikombe cha riadha wavulana mshindi wa pili.
Aidha mashindano haya yalifunguliwa na kufungwa na mgeni rasmi Katibu tawala wa mkoa (RAS) Bi. Karolina Mthapula
Katika upande wa Halmashauri ya mji Bunda, michezo hii ilikuwa ikiratibiwa na Ndugu Amos Mtani Afisa michezo akisaidiana na ndugu Liwina Mnamba Afisa michezo msaidizi. Jumla ya vikombe vilivyotwaliwa na Bunda Mji ni vikombe saba kati ya vikombe vyote vilivyoandaliwa katika mashindano haya.
Baadhi ya makocha ambao wamechaguliwa kupeleka timu Mtwara kwenye mashindano ya kitaifa toka Halmashauri ya mji Bunda ni Mwl.Robert Katabi akiwa anafundisha timu ya mpira wa miguu wanawake,Mwl. Mbahi Seruka akiwa anafundisha timu ya riadha, Mwl.Emmanuel Majura akiwa anafundisha timu ya mpira wa mikono na Mwl. Musa Rashid akiwa anaifundisha timu ya mpira wa kikapu. Walimu hawa walionesha bidii na maarifa katika kuziandaa timu zao hatimae kuleta ubingwa mkubwa katika halmashauri ya mji Bunda.
Hata hivyo Mgeni Rasmi katika mashindano hayo Bi.Karolina Mthapula aliwashukuru na kuwapongeza washiriki wote na washindi,pia aliwaasa wanamichezo na walimu waliochaguliwa kuunda timu hiyo ya MKoa wa Mara kuuwakilisha vyema Mkoa katika mashindano ya kitaifa huko Mkoani Mtwara.Mashindano hayo ya Taifa yanatarajiwa kuanza Tarehe 8/6/2019.

Subscribe to:
Posts (Atom)