Saturday, June 1, 2019

HALMASHAURI YA MJI BUNDA KINARA TENA UMISSETA 2019 MARA

Mashindano ya UMISSETA mkoa yalianza tarehe 29/05/2019 na kuhitimishwa tarehe 01/06/2019  katika viwanja vya shule ya sekondari Bunda. Mashindano haya yalihusisha halmashauri tisa za mkoa wa Mara ambazo ni Musoma manispaa,Musoma vijijini,Rorya,Bunda wilaya,Bunda Mji,Butiama,Tarime Mjini,Tarime vijijini na Serengeti.
Halmashauri zote hizi zilileta timu za michezo mbalimbali zikiwemo fani za ndani.
 Washindi mbalimbali toka halmashauri mbalimbali waliibuka na kujinyakulia zawadi kemkem zilizokuwa zimeandaliwa ikiwemo Vyeti na vikombe.
Halmashauri ya Bunda iliibuka kuwa bingwa wa Jumla katika mashindo ya mwaka huu ikiwa ni mara mbili mfululizo na kutwaa vikombe mbalimbali kama ifuatavyo kikombe cha mpira wa mikono wasichana na wavulana mshindi wa kwanza, kikombe cha mpira wa miguu wasichana mshindi wa kwanza, kikombe cha mpira wa kikapu wasichana mshindi wa kwanza, kikombe cha riadha wasichana mshindi wa kwanza, kikombe cha kikapu wavulana mshindi wa pili na kikombe cha riadha wavulana mshindi wa pili.
Aidha mashindano haya yalifunguliwa na kufungwa na mgeni rasmi Katibu tawala wa mkoa (RAS) Bi. Karolina Mthapula
Katika upande wa Halmashauri ya mji Bunda, michezo hii ilikuwa ikiratibiwa na Ndugu Amos Mtani Afisa michezo akisaidiana na ndugu Liwina Mnamba Afisa michezo msaidizi. Jumla ya vikombe vilivyotwaliwa na Bunda Mji ni vikombe saba kati ya vikombe vyote vilivyoandaliwa katika mashindano haya.
Baadhi ya makocha ambao wamechaguliwa kupeleka timu Mtwara kwenye mashindano ya  kitaifa toka Halmashauri ya mji Bunda ni Mwl.Robert Katabi akiwa anafundisha timu ya mpira wa miguu wanawake,Mwl. Mbahi Seruka akiwa anafundisha timu ya riadha, Mwl.Emmanuel Majura akiwa anafundisha timu ya mpira wa mikono na Mwl. Musa Rashid akiwa anaifundisha timu ya mpira wa kikapu. Walimu hawa walionesha bidii na maarifa katika kuziandaa timu zao hatimae kuleta ubingwa mkubwa katika halmashauri ya mji Bunda.
Hata hivyo Mgeni Rasmi katika mashindano hayo Bi.Karolina Mthapula aliwashukuru na kuwapongeza washiriki wote na washindi,pia aliwaasa wanamichezo na walimu waliochaguliwa kuunda timu hiyo ya MKoa wa Mara kuuwakilisha vyema Mkoa katika mashindano ya kitaifa huko Mkoani  Mtwara.Mashindano hayo ya Taifa yanatarajiwa kuanza Tarehe 8/6/2019.












No comments:

Post a Comment