Wednesday, June 6, 2018

BUNDA TC (Bunda Mji)KINARA MASHINDANO YA 39 UMISSETA MKOA WA MARA.

 

Mgeni Rasmi siku ya uzinduzi (Wa katikati wenye sare)

  Bunda mji yaibuka mshindi wa jumla katika mashindao ya UMMISETA mkoa wa Mara kwa kujinyakulia kombe la jumla.Mashindano hayo yaliyofanyika katika sekondari Bunda ya sekondari Bunda (Bunda high school),yalifunguliwa mnamo tarehe 27/05/2018 na Katibu tawala Mkoa wa Mara na kufungwa tarehe 29/05/2018.

Mgeni Rasmi siku ya Kufunga mashindano (Mwenye suti na kivalio chekundu ndani) akiwa katika zoezi la ugawaji zawadi mbali mbali kwa washindi.


                         
Kombe la jumla walilokabidhiwa Bunda Mji baada ya kuibuka vinara katika mashindano hayo.
                           




Afsia elimu sekondari (DEO) Bunda mji Bw.Nyamhanga akiwa baadhi ya Zawadi na kombe la Jumla mezani.





    Ambapo jumla ya wanamichezo  120 toka katika halmashauri tisa (9) za mkoa wa Mara zilishiriki kwa michezo mbali mbali ikiwemo Mpira wa miguu kwa wasichana na wavulana,mpira wa pete,riadha,kwaya,handball,volleyball n.k.

     Wanamichezo hao waliondoka Katika kambi ya Mkoa iliyokua chini ya uangalizi wa makocha mahili kwa kila timu iliyochaguliwa kuelekea Jijini Mwanza kuungana na wenzao toka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani kwa ajili ya michezo hiyo ngazi ya Taifa iliyoanza Tarehe 03/06/2018.

 
     Halmashauri hizo tisa ni pamoja na Bunda Mji (wenyeji),Bunda wilaya,Butiama,Tarime mji,Tarime wilaya,Rorya,Serengeti,Musoma manispaa na Musoma wilaya.







  Hata hivyo Afisa michezo Mkoa wa Mara Bw.Evance Sangawe aliwaahidi wanamichezo na viongozi waliochaguliwa kutoa ushirikiano wa kutosha wa hali na mali ili Timu toka mkoa wa Mara ziweze kurudi na Vikombe na zawdi nyingine za kutosha tofauti na miaka iliyopita.

Afisa michezo mkoa wa Mara Bw.Evance Sangawe (kushoto) akiwa na Mkuu wa shule ya sekondari Bunda Bw.Machota Kora.

No comments:

Post a Comment