Thursday, June 6, 2019

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO TOKA NA KUJIUNGA BUNDA SECONDARY SCHOOL 2019/2020

WALIOCHAGULIWA TOKA BUNDA SECONDARY SCHOOL 2019/2020Tunapenda kuwapongeza vijana wetu wote waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano kwa tahasusi mbali mbali,pia wale waliochaguliwa kujiunga na vyu mbali mbali na bila kuwasahau wale ambao hawajachaguliwa na wakaamua kujiunga na masomo ama vyuo mbalimbali binafsi,tunaamini watafanya vizuri huko waendako.Na kwa wale mlioamua kuikamilisha safari ya Elimu na kuamua kujiunga na shughuli mbali mbali za ujasiliamali nanyi pia tunawatakia kila lakheri.



Kwa wale mliochaguliwa kujiunga na Bunda secondary kwa tahasusi zetu za HGK,HGK na EGM karibuni sana,Bunda secondary ni kisima cha maarifa hakika hamtatoka kama mlivyokuja tunawakaribisha sana.Kwa taarifa zaidi wasiliana na uongozi wa shule ama kwa Barua pepe bundahighschool@gmail.com
Mzazi mlezi mlete mwanao aliyechaguliwa Bunda secondary maana kwetu " NIDHAMU NI USHINDI"
WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA BUNDA SECONDARY KIDATO CHA TANO 2019/2020











Nanyi mliopita Bunda secondary tunaamini huko mliko mnaendelea kua mabalozi wazuri wa shule yetu pendwa kwa kuitangaza kwa mazuri yote.
 

3 comments:

  1. Napenda kuwapa hongera wadogo zangu kwa juhudi zao walizozionyesha sasa Mungu awatangulie huko muendako mkawe vichwa kama jinsi Mungu alivyotuagiza,,


    Kwa wapendwa waliochaguliwa Bunda High School karibuni sana kwani hata sisi tumetoka hapo na sasa tuko vyuo tofautitofauti hapa Tanzania na wengine nje ya Tanzania.

    Baba wa mbinguni na atuangazie nuru

    Our motto: discipline is our victory.

    ReplyDelete
  2. Hongereni sana wadogo zangu waliochaguliwa kuendelea na masomo ya advance MUNGU awatangulie Sana lakini pia nipende kuwapa pongezi kwa wale wote waliobahatika kupata nafasi ya kujiunga na shule yetu hakika mmepata kituo sahihi chenye maarifa kwa ajili ya wanafunzi pia MUNGU awatangulie katika masomo yenu

    ReplyDelete
  3. Mmi sharifu maarifa nimefurah kuja bunda

    ReplyDelete