Thursday, July 18, 2019

HONGERENI KIDATO CHA SITA 2014/2016

Kila lenye mwanzo halikosi mwisho,tunaungana na ndugu,jamaa na marafiki kuwapongeza vijana wetu wa kwanza kabisa mlioifungulia njia Bunda sekondari kwa Kidato cha tano mnamo mwaka 2014,ambao baadhi yenu mlijiunga na elimu ya juu katika vyuo mbali mbali mwaka 2016 kama vile SAUT,UDSM,IFM,CBE,UDOM n.k. mkisoma kozi mbali mbali.
Tunaamini wengi wenu hasa wale mliosoma kozi za miaka mitatu mtakua mnamalizia mitihani yenu na wengine tayari mmeishamaliza tunawapongeza sana.
Elimu mliyoipata itakua na manufaa kwenu na kwa jamii pia,maana kuna Walimu,wahasibu,Waandishi wa habari,wanasheria n.k. ambao jamii inawategemea kwa namna moja ama nyingine.
Mbali na changamoto za kuajiliwa muda mliokaa shuleni bila shaka mmejifunza mbinu na njia mbalimbali zitakazowafanya kua na uwezo wakujiari.
Tusiwasahau pia ambao mliamua kujiunga na Vyuo mbali mbali kwa ngazi za Astashahada na stashahada ambao mmlimaliza au manamaliza hivibkaribuni nanyi pia hongereni sana.
Kuna kundi la wale ambao hamkupenda kuendelea na masomo mkajiingiza kwenye shughuli za ujasiliamali tunaamini mlichagua njia sahihi ya kujikwamua kimaisha tunawapongeza pia..
Tunawaomba popote pale mlipo na mtakapokua
endeleni kua mabalozi wazuri wa shule na vyuo mlivyosoma,tambueni kua kua nidham siku zote itabaki kua ni ushindi,heshimuni kila mtu bila kujali jinsia,hali ya uchumi,rangi wala kabila,maana bado mko katika mapambano ya utafutaji.
Mwisho kabisa tunawatakia kila lakheri katika harakati huko mitaani kunakowasubiri kwa amani Mungu awabariki sana.

1 comment: