BUNDA SECONDARY SCHOOL FORM FIVE JOINING INSTRUCTION 2021/2022
BUNDA - HIGH - SCHOOL (BHS)
BLOGU HII NI MAALUM KWA MASUALA YA TAALUMA YAHUSUYO BUNDA SEKONDARI.MAONI YENYE LUGHA ZISIZO NZURI YATAONDOLEWA.KARIBUNI KWA MAONI NA USHAURI. "NIDHAMU NI USHINDI"
Saturday, June 5, 2021
FORM FIVE JOINING INSTRUCTION BUNDA SECONDARY SCHOOL 2O21
Saturday, January 16, 2021
MATOKEO KIDATO CHA NNE NA PILI 2020
🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓🎓
Uongozi wa Shule unawapongeza kwa dhati kwa matokeo haya wanafunzi wetu wa kidato cha Nne 2020.Mungu na awatangulie katika safari yenu ya kitaaluma kwa wale mtakaoyatumia kujiendeleza kielimu zaidi na hata wale mliofanya vibaya msikate tamaa maana bado mnayo fursa kubwa sana katika maisha.
Shukran kwa Walimu,wazazi na wale wote walioshirikia katika kuhakikisha Bunda Secondary inazidi kupanda juu zaidi katika taaluma.Hakika matokeo haya yatakua ni chachu ya kuboresha zaidi na zaidi taaluma ya shule yetu.
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏
PONGEZI nyingi ziwaendee wanafunzi wa kidato cha pili ambao nao pia kwa juhudi kubwa wamefanya vizuri.Tunawakaribisha tena kwa Mikono miwili katika kuendelea na Ngwe nyingine tena kwa masomo ya Kidato cha tatu Tunawaahidi kua nanyi bega kwa bega katika kuwaandaa ili mje kufanya vyema kabisa katika mtihani wenu mwakani.Maana siku zote MAVUNO yaliyobora hutokana na MAANDALIZI yaliyobora Pia.TUNAWAPENDA SANA.
Mwisho kabisa Pongezi za kutosha ziwaendee WALIMU,WAZAZI/WALEZI na washika dau wote walioshikana nasi Bega kwa bega mpaka hapa tulipo.Mchango wenu bado unahitajika sana.
TUNASEMA NIDHAMU NI USHINDI NA MAPAMBANO YANAENDELEA.
UNGANA NASI KATIKA UKURASA WETU WA FACEBOOK
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏
Wednesday, June 24, 2020
PONGEZI
Tunaamini mtafanya vizuti katika ngazi hiyo ya Elimu.Bila kuwasahau wale wote mliokosa nafasi ya kuendelea na elimu tunaamini Nanyi pia hamtakata tamaa katika Kuitafuta elimu kwa namna moja ama nyingine.
Siku zote kaeni mkiamini NIDHAMU NI USHINDI.
Kila lakheri kwenu Nyote na Mungu awabariki sana.
Saturday, June 13, 2020
WELCOME/KARIBU
Shule hii ina kidato cha kwanza hadi cha sita kwa tahasusi tatu HGK,HGK NA EGM,pia hapa utapata matukio mbalimbali yahusuyo Shule yetu ya sekondari Bunda,elimu na mambo ya taaluma pia picha za matukio nayo.
Tuesday, January 28, 2020
Thursday, July 18, 2019
HONGERENI KIDATO CHA SITA 2014/2016
Tunaamini wengi wenu hasa wale mliosoma kozi za miaka mitatu mtakua mnamalizia mitihani yenu na wengine tayari mmeishamaliza tunawapongeza sana.
Elimu mliyoipata itakua na manufaa kwenu na kwa jamii pia,maana kuna Walimu,wahasibu,Waandishi wa habari,wanasheria n.k. ambao jamii inawategemea kwa namna moja ama nyingine.
Mbali na changamoto za kuajiliwa muda mliokaa shuleni bila shaka mmejifunza mbinu na njia mbalimbali zitakazowafanya kua na uwezo wakujiari.
Tusiwasahau pia ambao mliamua kujiunga na Vyuo mbali mbali kwa ngazi za Astashahada na stashahada ambao mmlimaliza au manamaliza hivibkaribuni nanyi pia hongereni sana.
Kuna kundi la wale ambao hamkupenda kuendelea na masomo mkajiingiza kwenye shughuli za ujasiliamali tunaamini mlichagua njia sahihi ya kujikwamua kimaisha tunawapongeza pia..
Tunawaomba popote pale mlipo na mtakapokua
endeleni kua mabalozi wazuri wa shule na vyuo mlivyosoma,tambueni kua kua nidham siku zote itabaki kua ni ushindi,heshimuni kila mtu bila kujali jinsia,hali ya uchumi,rangi wala kabila,maana bado mko katika mapambano ya utafutaji.
Mwisho kabisa tunawatakia kila lakheri katika harakati huko mitaani kunakowasubiri kwa amani Mungu awabariki sana.