Kila lenye mwanzo halikosi mwisho,tunaungana na ndugu,jamaa na marafiki kuwapongeza vijana wetu wa kwanza kabisa mlioifungulia njia Bunda sekondari kwa Kidato cha tano mnamo mwaka 2014,ambao baadhi yenu mlijiunga na elimu ya juu katika vyuo mbali mbali mwaka 2016 kama vile SAUT,UDSM,IFM,CBE,UDOM n.k. mkisoma kozi mbali mbali.
Tunaamini wengi wenu hasa wale mliosoma kozi za miaka mitatu mtakua mnamalizia mitihani yenu na wengine tayari mmeishamaliza tunawapongeza sana.
Elimu mliyoipata itakua na manufaa kwenu na kwa jamii pia,maana kuna Walimu,wahasibu,Waandishi wa habari,wanasheria n.k. ambao jamii inawategemea kwa namna moja ama nyingine.
Mbali na changamoto za kuajiliwa muda mliokaa shuleni bila shaka mmejifunza mbinu na njia mbalimbali zitakazowafanya kua na uwezo wakujiari.
Tusiwasahau pia ambao mliamua kujiunga na Vyuo mbali mbali kwa ngazi za Astashahada na stashahada ambao mmlimaliza au manamaliza hivibkaribuni nanyi pia hongereni sana.
Kuna kundi la wale ambao hamkupenda kuendelea na masomo mkajiingiza kwenye shughuli za ujasiliamali tunaamini mlichagua njia sahihi ya kujikwamua kimaisha tunawapongeza pia..
Tunawaomba popote pale mlipo na mtakapokua
endeleni kua mabalozi wazuri wa shule na vyuo mlivyosoma,tambueni kua kua nidham siku zote itabaki kua ni ushindi,heshimuni kila mtu bila kujali jinsia,hali ya uchumi,rangi wala kabila,maana bado mko katika mapambano ya utafutaji.
Mwisho kabisa tunawatakia kila lakheri katika harakati huko mitaani kunakowasubiri kwa amani Mungu awabariki sana.
BLOGU HII NI MAALUM KWA MASUALA YA TAALUMA YAHUSUYO BUNDA SEKONDARI.MAONI YENYE LUGHA ZISIZO NZURI YATAONDOLEWA.KARIBUNI KWA MAONI NA USHAURI. "NIDHAMU NI USHINDI"
Thursday, July 18, 2019
Sunday, July 14, 2019
KILA LA KHERI KIDATO CHA NNE.
Tunapenda kuungana na wazazi,walezi,ndugu,jamaa na marafiki katika kuwatakia kila la kheri wanafunzi wetu wa kidato cha nne wanaoanza leo mitihani ya Utimilifu "Mock" mkoa wa Mara.Tunaamini kwa uwezo wake Mungu Ufaulu utaongezeka.
Thursday, July 11, 2019
MATOKEO KIDATO CHA SITA 2019
https://matokeo.necta.go.tz/acsee/acsee.htm
Tunapenda kuwapongeza wanafunzi wetu kwa matokeo haya.
MATOKEO BUNDA SECONDARY Pdf
Monday, July 8, 2019
KARIBUNI TENA.
Ikiwa leo tarehe 8/7/2019 shule zinafunguliwa,tunapenda kuwakaribisha sana wanafunzi wanaoanza Muhula wa Pili kwa wale wa kidato cha Kwanza hadi cha Nne Na kwa wale mnaoanza kidato cha sita karibu sana Mungu awabariki sana Katika safari yenu ya taaluma.
Pia tuwakaribishe sana kidato cha Tano.
Mbali na yote tujikumbushe kwa wale mliopita Bunda Secondary,Wewe ni wa utawala wa mkuu gani kati ya hawa pichani?
Pia tuwakaribishe sana kidato cha Tano.
Mbali na yote tujikumbushe kwa wale mliopita Bunda Secondary,Wewe ni wa utawala wa mkuu gani kati ya hawa pichani?
Subscribe to:
Posts (Atom)